Natural Bliss

106. NJIA ZA KUZUIA/KUONDOA MBA KICHWANI

Mba kwa kiasi kikubwa hutokana na ukavu wa ngozi au fungus ambao hutokana na cell za ngozi ya kichwa zilizo kufa. 

Mba hutia aibu na wengi hufikiri mba hutokana na uchafu pale unapokuna kichwa mbele za watu; 99% ya watu hao watajua nywele zako ni chafu hujaosha japo kuwa mba pia huweza kusababishwa na aina ya mafuta unayotumia.

Hizi ni njia chache ambazo zinatumia viungo vya nyumbani/jikoni kutoa mba kirahisi sana

🧚‍♂️Vinegar/Siki: 

Husaidia kuua fungus na bacteria wanoa sababisha mba.

-Osha kichwa chako/ngozi ya kichwa kwa kutumia shampoo isiyo na viambata sumu.

-Chukua siki changanya na maji kidogo paka katika ngozi ya kichwa 

-Kaa na mchanganyiko huo kwa muda wa lisaa limoja kisha osha kichwa chako.

🧚‍♂️Baking Soda: 

Husaidia kuondoa cell za ngozi zilizo kufa 

-Changanya baking soda kidogo katika shampoo yako kisha utumie kuoshea nywele zako.

🧚‍♂️Vitunguu swaumu:

Saga vitunguu swaumu changanya na asali na tangawizi ili kukata ile harufu mbaya ya kitunguu swaumu paka kwenye ngozi ya kichwa kaa nayo kwa muda wa nusu saa kisha osha nywele zako. 

-Unaweza pia kutumia shampoo au conditioner zenye kitunguu swaumu (Hakikisha hazina viambata vingine ambavyo ni hatarishi kwa nywele zako).

🧚‍♂️Aloe vera:

Chukua jani la Aloe Vera saga changanya na maji kidogo paka kwenye ngozi ya kichwa kaa nayo kwa muda wa lisaa kisha osha nywele zako.


🧚‍♂️Tumia rafiki kwa nywele na ngozi ya kichwa, Mafuta yasiyoganda kwenye ngozi ya kichwa au nywele zako. Hapa inashauriwa zaidi kutumia mafuta ya maji kama vile castor oil, Olive oil, jojoba oil, coconut oil nk

Post a Comment

0 Comments