📌Je katika ratiba zako za utunzaji nywele umewaza kuhusu kipengele cha matumizi ya Proteins? (Protein treatment au Protein Therapy).
Leo tutajifunza faida zake na nywele ikikosa lishe hii itakuaje.
Twende pamoja😊
Protein Treatment husaidia;
🧚♂️Kutunza unyevu na kuzifanya nywele kuwa nzito
-Mara nyingi nywele ikikosa protein huwa nyepesi sana na kupoteza ule uhalisia wake.
🧚♂️Husaidia kuziba mapengo yaliyowazi na kusaidia maeneo yaliyo yaliyodhoofika.
🧚♂️Kupunguza nywele kuwa nyembamba na kukatika ovyo
🧚♂️Kuimarisha nywele zilizoharibika kwa moto,rangi za nywele au Madawa(Relaxer)
🧚♂️Kuipa nywele kiwango sahihi cha protein na lishe kwa nywele zako
🧚♂️Kuzia nywele kubadilika rangi
📌Kumbuka kuzipa nywele zako proteins kabla na baada ya mitindo kinga hasa rasta au mitindo ya muda mrefu
📌Zingatia muda sahihi wa kuipa nywele zako protein ni kila wiki 4/6/8 inategemea na udhaifu ya nywele zako.
Je leo umefahamu kwanini nywele zako zinahitaji protein?au zikikosa protein zinakuaje?
0 Comments