Natural Bliss

109. FAIDA ZA KUSTEAM/KUZIPA NYWELE JOTO/MVUKE KWA KUTUMIA STEAMING CAP/STEAMER


Kitu ambacho watu wengi husahau au kukidharau au kukipuuzia ni kuzipa nywele joto wakati wa kufanya steaming. Unaweza kutumia heating/Steaming caps au steamer.

Faida kubwa zaidi ya kuzipa nywele joto ni fungua hair cuticles ambazo zinarahisisha upokeaji wa products.

Watu wengi wanapenda kupaka mafuta au butter kwa wingi wakijua ndio wanatunza nywele vizuri, lakini uhalisia ni kufanya steaming ndio kuna moisturize nywele vizuri na kufanya nywele ikue na kunawiri vizuri.

Kupaka mafuta au products nyingi bila kufanya steaming au protein treatment kunafanya nywele ziwe kavu sana, kupoteza unyevu haraka zaidi na kukatika au hair shedding inakua kubwa sana. 

Kukaa mwezi mmoja bila kufanya steaming ni kosa sana kwa naturalistars/watu wanaotunza nywele za asili. Kwa hiyo baada ya kuosha nywele, ukishapaka steaming kwenye nywele vaa steaming cap yako kama kwenye video hapo chini halafu baada ya kumaliza utaosha nywele kwa maji safi (bila shampoo).




Hakikisha umefanya steaming kabla hujasuka nywele za kukaa nazo mwezi au miezi miwili kuzuia nywele kukatika na kuwa nyepesi sana.

Ukihitaji steaming caps/Kofia kwa ajili ya kufanyia steaming zipo kwetu kwa Tshs 25,000/= tu

📞0672 765 929

Post a Comment

0 Comments