Natural Bliss

110. JINSI YA KUTUNZA NYWELE AMBAZO NI LOW POROSITY


 🧚‍♂️Usitumie bidhaa yoyote ambayo ina silicone.

🧚‍♂️Jitahidi kutumia moto/mvuke au steamer (heating) wakati unafanya steaming / deep conditioning

🧚‍♂️Jitahidi kutokutumia bidhaa nyingi sana kwa wakati mmoja (Zipe nywele zako muda wa kuzoea bidhaa moja kabla ya kubadili kwenda bidhaa nyingine. Hapa naongelea bidhaa ambazo zinafanya kazi moja kama vile Shampoo au Conditioner.

🧚‍♂️Tumia mafuta mepesi kama vile Mafuta ya parachichi (Avocado oil), Mafuta ya almond (Almond oil) au Mafuta ya mzeituni (Olive oil)

🧚‍♂️Siku zote tumia njia ya LCO (LCO method) wakati unapaka products zako.

       ☘️L = Leave in Conditioner (Hii inatikiwa iwe ya kwanza kabisa kupaka baada ya kuosha nywele wakati nywele bado ina unyevu unyevu.

      ☘️C = Cream (inaweza kuwa shea butter au cream nyingine ya nywele) hii inasaidia kushikilia unyevu ambao umepokewa na Leave in Conditioner

      ☘️O = Oil/Mafuta (hapa unapaka mafuta ili kulainisha zaidi nywele) 


Hizi products zote zinapakwa kuanzia kwenye shina la nywele hadi kwenye ncha za nywele (Yaani unapaka nywele zote).


🧚‍♂️Tumia Clarifying shampoo, hakikisha shampoo ambayo unatumia imeandikwa hivyo au ni ile ambayo imekua designed kuondoa uchafu zaidi.

🧚‍♂️Wakati unaosha nywele jitahidi kutumia maji ya vuguvugu (Warm water), usitumie maji ya baridi kabisa.

🧚‍♂️Usitumie sana bidhaa zenye protein nyingi.

🧚‍♂️Tumia bidhaa ambazo ni water based, kama vile Leave in conditioners, bidhaa za kustyle nywele nk

🧚‍♂️Tumia bidhaa sahihi kwa ajili ya nywele ambazo ni low porosity

🧚‍♂️Jaribu kuepuka matumizi ya moto wakati wa kustyle nywele; kama vile matumizi ya pasi, dryers nk 


Ukihitaji Leave in Conditioners, Shea butter, Mafuta ya nywele aina zote; Tupigie au WhatsApp namba hii: 0672 765 929

Post a Comment

0 Comments