Natural Bliss

111. JINSI YA KUONDOA NA KUZUIA MBA KWENYE NYWELE

 


Mba ni nini??

Mba ni hali ambayo kwa sasa imekua na kawaida kuwasumbua watu wengi, hali hii hutambulishwa na kuongezeka kwa  ngozi nyembamba ya kichwa juu ya ngozi ya kawaida.


SABABU ZA MBA (NINI HUSABABISHA KUPATA MBA)

☘️Seborrheic Dermatitis: Aina hii hutambulishwa kwa kuvimba na kutokea kama wekundu kwenye ngozi, pia kujaa kwa vitu kama ukoko au magamba kwenye ngozi. Hali hii hushambulia zaidi sehemu zenye mafuta mengi kama vile ngozi ya kichwa, usoni na upande wa juu wa kifua.


☘️MalasseziaHii ni aina ya fungus ambayo husababisha maambukizi na kuvimba.Fungus hizi hutumia mafuta ya asili (Natural oils) kama chakula na kusababisha ngozi ya kuchwa kuwa kavu na nyembamba sana; hali hii huongeza chance za kupata mba.


☘️Dry scalp (Ngozi ya kichwa kuwa kavu): Ngozi ya kichwa ambayo ni kavu sana au ina unyevu kidogo hupelekea kuvimba, kuwasha na kuchoma choma. Hali hiyo husababisha ngozi ya kichwa kuwa nyembamba na mwisho kupata mba.


JINSI YA KUONDOA MBA/ UNAWEZAJE KUONDOA MBA KICHWANI

🧚‍♂️Osha nywele zako mara kwa mara: Mkusanyiko wa uchafu, mafuta na ngozi iliyokufa huongeza uwezekano wa kupata mba.

🧚‍♂️Usitumie shampoo ambayo husababisha ngozi ya kichw kukauka, inaweza pelekea tatizo kuwa kubwa zaidi.

🧚‍♂️Tumia shampoo ambazo ni anti-Dandruff (anti-mba), hizi mara nyingi zinakua zina salicyclic acid, ketoconazole, zinc pyrithione, and selenium sulfide ambazo huzuia kutengeneza build up ambayo baadae husababisha mba. 

🧚‍♂️Badili mfumo wako wa chakula. Kulingana na utafiti inaonesha kuwa vyakula vyenye mafuta na sukari sana husababisha kupata mba zaidi kuliko vyakula ambavyo vinaunda mlo kamili.

🧚‍♂️Hakikisha unascrub (kufanyia exfoliation) ngozi ya kichwa kuondoa ngozi iliyokufa na product build ups.


UKIHITAJI MAFUTA YA MAJI MAZURI , SHAMPOO ZISIZO NA VIAMBATA SUMU, SHEA BUTTER...TUPIGIE AU WHATSAPP: 0672 765 929


TUTAENDELEA POST INAYOFUATA....

Post a Comment

0 Comments