Natural Bliss

112. JINSI YA KUONDOA NA KUZUIA MBA UKIWA NYUMBANI KWAKO (Home Remedies)



 🧚‍♂️Juice ya limao

Mahitaji


  • 2 tbsp maji/juice ya tangawizi
  • 3 tbsp mtindi
  • 1 tbsp maji ya limao/ndimu


Jinsi ya kuandaa

  • Changanya mahitaji yako yote.
  • Paka mchanganyiko huu kwenye ngozi ya kichwa.
  • Uache mchanganyiko kwa dakika 10 hadi 15
  • Osha nywele na shampoo
  • Rudia process hii at least mara 1-2 kwa wiki.  

🧚‍♂️Tea trea oil

Tea trea oil ina tabia za kuzuia kuvimba na maambukizi yoyote (anti-inflammatory and antimicrobial properties) ambazo husaidia kutibu na kuzuia kupata mba.


Mahitaji:

  • Matone 2-3 ya mafuta ya maji

Jinsi ya kuandaa

  • Changanya tea tree oil na mafuta ya maji.
  • Lowanisha pamba kwa kutumia mchanganyiko huo halafu paka kwenye ngozi ya kichwa.
  • Rudia process hii angalau mara 3-4 kwa wiki.



🧚‍♂️Mafuta ya maji

Hapa ni muhimu kutumia mafuta ambayo ni mepesi (yana Low molecular weight), haya yatasaidia kunourish na kucondition nywele zako pia yataongeza unyevu kwenye nywele na ngozi ya kichwa hivyo kuondoa ukavu ambao unaweza kupelekea kupata mba.


Mahitaji

  • 2 tbsp mafuta ya maji


Jinsi ya kuandaa

  • Massage mafuta yako ya maji kwenye ngozi ya kichwa
  • Acha kwa nusu saa hadi lisaa 
  • Osha nywele na shampoo isiyo na viambata sumu
  • Rudia process hii walau mara 2 kwa wiki


🧚‍♂️Aloe vera

Aloe vera ina tabia za kuzuia kuvimba na maambukizi yoyote (anti-inflammatory and antimicrobial properties) ambazo husaidia kutibu na kuzuia kupata mba.

 

Mahitaji

  • Aloe vera gel


Jinsi ya kuandaa

  • Massage aloevera gel kwenye ngozi ya kichwa hadi ipotee kabisa
  • Acha nywele zako kwa lisaa, halafu osha.
  • Rudia process hii walau mara 2 kwa wiki


🧚‍♂️Apple Cider Vinegar

Apple cider vinegar huwa ina  acetic acid ambayo inasaidia kubalance pH level ya ngozi ya kichwa, Hii husaidia kuzuia ngozi ya kichwa kupoteza unyevu na kukauka sana hali ambayo hupelekea mtu kupata mba.


Mahitaji

  • 1 tbsp ya raw apple cider vinegar (ACV).
  • 3 tbsp ya maji masafi. 


Jinsi ya kuandaa

  • Changanya raw apple cider vinegar na maji.
  • Paka mchanganyiko huu kwenye ngozi ya kichwa.
  • Uache mchanganyiko kwa dakika 10 hadi 15
  • Osha nywele na shampoo
  • Rudia process hii at least mara 1-2 kwa wiki.  



🧚‍♂️Juice ya Kitunguu maji

Kitunguu pia kina anti-fungal properties ambayo huzuia ukuaji wa malassazia furfur.


Mahitaji

  • Kitunguu maji kimoja kikubwa
  • Maji masafi


Jinsi ya kuandaa

  • Blend kitunguu na upate juice yake
  • Changanya juice na mafuta ya maji kidogo
  • Paka mchanganyiko kwenye ngozi ya kichwa
  • Acha mchanganyiko kwa dk 45 hadi lisaa
  • Osha nywele zako vizuri
  • Rudia hii walau mara mbili kwa wiki.


UKIHITAJI MAFUTA YA MAJI MAZURI TUPIGIE AU WHATSAPP: 0672 765 929


TUTAENDELEA POST INAYOFUATA....

Post a Comment

0 Comments